Tanclick Company Limited ni daraja kati yako na wateja wako watarajiwa. Kupitia mfumo wetu wa DCCS, tunakuunganisha na watu wanaohitaji huduma zako kwa ufanisi mkubwa.
Tanclick Company Limited ni kampuni ya kitaalamu inayotoa suluhisho za kisasa za masoko. Tunajikita katika kusaidia wafanyabiashara kupata wateja halisi kwa njia ya moja kwa moja, ya haraka na yenye matokeo.
Tofauti na wengine, sisi hatufanyi majaribio na biashara yako. Tunatumia uelewa mpana wa tabia za wateja na data ili kuhakikisha kila hatua tunayochukua inaleta faida inayoonekana.
Mfumo wa kisasa unaoondoa kubahatisha. Tunatumia data na teknolojia kukuunganisha na soko lako moja kwa moja.
Hatupigi ramli. Tunachambua data kubaini nani anahitaji bidhaa yako sasa hivi, na yuko wapi.
Tunakutambulisha kwa mteja kwa weledi. Ujumbe wako unafika kwenye simu zao moja kwa moja.
Unapata nafasi ya kuuza na kujenga uaminifu. Matokeo ni mauzo yanayokua na biashara imara.
Hatua 4 rahisi za kitaalamu kuelekea mafanikio ya biashara yako.
Tunafanya uchambuzi wa kina kuelewa biashara yako, bidhaa zako, na changamoto zako za sasa.
Tunatengeneza mfumo wa "Laser Targeting" ili kuwapata wateja wenye njaa ya bidhaa zako.
Tunawaingiza wateja wapya moja kwa moja kwenye mfumo wako wa mauzo kwa njia ya kisasa.
Unapokea wateja, unafunga mauzo, na tunakupa ripoti kamili ya matokeo ya kazi yetu.
Mfumo wetu wa DCCS umeundwa kuleta wateja ndani ya muda mfupi baada ya kuanza kampeni.
Hatuleti namba tu; tunawaleta watu ambao tayari wana nia ya kununua unachouza.
Tunatoa suluhisho zinazoendana na bajeti yako huku tukihakikisha faida kubwa (High ROI).
Timu yetu itakuongoza jinsi ya kuzungumza na wateja ili uweze kufunga mauzo mengi zaidi.
Kila hatua inayopigwa utapewa ripoti kamili ili uone thamani ya kila shilingi unayowekeza.
Tuko hapa kwa ajili yako muda wowote unapohitaji ufafanuzi au mabadiliko ya mkakati.
"Kabla ya kuanza na Tanclick kupitia mfumo wa DCCS, tulikuwa tunatumia pesa nyingi kwenye matangazo bila kupata wateja. Ndani ya mwezi mmoja, tumeweza kuunganishwa na wateja wakubwa wa ujenzi ambao hatukuwatarajia."
"Uwezo wao wa kuelewa soko la Kitanzania ni wa kipekee. Wametusaidia kupata wateja halisi wa jumla kwa ajili ya bidhaa zetu za ngozi. Huduma yao ni ya kuaminika na ina matokeo ya haraka sana."
"Nimevutiwa sana na uwazi wao. Wanatoa ripoti za kila hatua na wateja wanatuita wenyewe kuulizia huduma. Huu ni uwekezaji bora zaidi nilioufanya kwa biashara yangu mwaka huu."